shuka nayo
WHY ME_________(13)
Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
Stephano alianza kutetemeka huku akizidi kumuomba mungu na kukumbuka maneno ambayo aliambiwa usiku wa jana.
"Kijana umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana, nyumba hii ukiingia basi usahau kabisa kama utatoka mzima"
Maneno yale na tukio lile vikamfanya azidi kuchanganyikia.
SHUKA NAYO SASA
Alikaa kimya na kujifanya kufumba macho, akajifanya kama hakuliona lile tukio lililotokea.
Alifika mpaka pale ambapo yupo stephano na kumuangalia kisha akavua mawani yake na kuishika mkononi na kuchuchumaa chini, alikaa kimya kwa sekunde chache kisha akaongea kwa sauti ya upole.
"Kijana unatatizo gani? mbona hupo hapa?"
Swali lile lilizidi kumchanganya Stephano ambaye hakufahamu chochote aliongea huku machozi yakiwa yanamtoka
"Sijui chochote nilishangaa nimekamatwa na kuletwa hapa na kukutana na sura ngeni machoni mwangu"
Baada ya kuongea maneno yale jamaa ambaye alikuwa anamuhoji stephano alicheka kwa sauti ya juu sana kitendo ambacho kilimfanya Stephano azidi kuingiwa na uwoga alipomaliza kucheka aliongea maneno ambayo yalimuacha na maswali stephano.
"Kijana ukiletwa hapa ujue kuna kosa umerifanya, huwezi ukaletwa kama mtarii na siku zako za kuishi zinahesabika"
Alipomaliza kuongea maneno yale aliondoka eneo lile ambalo alikuwepo stephano na kwenda kwa wenzake kisha akazungumza nao kwa ishara na wote watatu walicheka kisha wakatoweka eneo lile.
Baada ya dakika tano waliingia vijana wanne na kuubeba mwili wa yule kijana ambaye aliuwawa, maswali hayakumuisha kichwani mwake kila akijaribu kuangalia mazingira ya mule alikuwa hayaelewi kabisa.
Masaa machache baadaye alikuja kijana mmoja na mwanadada ambao walivaa kinadhifu na kufika mpaka pale ambapo alikuwa Stephano.
Walimfungua kamba ambazo alikuwa amefungwa kwenye mikono kisha wakamnyanyua na kumuingiza kwenye chumba ambacho alikutana na watu ambao wote walikuwa wamevaa suti nyeusi na mawani meusi, Stephano aligeuza macho kwa uwoga alizidi kuchanganyikiwa sekunde chache wale watu ambao wamemleta Stephano wakatoweka na kumuacha Stephano peke yake kwenye kundi lile la watu ambao muda wote sura zao zilikuwa zinaonyesha wazi wazi kuwa sio watu wakawaida..
Ukimya ulitawala kwa dakika chache kitendo ambacho kilizidi kumchanganya dakika chache baadaye bwana mmoja ambaye mwili wake ulikuwa umejaa kutokana na mazoezi ya nguvu ambayo anayafanya alinyanyuka na kumfata Stephano, Stephano alipomtazama kwa umakini akakumbuka kuwa ndiye yule ambaye alitoa hukumu ya kifo kwa kijana ambaye hakuweza kujua maiti ya yule kijana imepelekwa wapi.
Alimsogelea mpaka pale kisha akaongea kwa sauti ya upole saana
"Kijana, nakuonea huruma sana hivi ulikosa wanawake mpaka ukatembee na mtoto wa boss wangu"
Maneno yale ndiyo ambayo yalimfungua masikio Stephano na kufahamu kuwa Anna ndio chanzo cha matatizo yote, Mapigo ya moyo yalizidi kwenda kasi huku kijasho chembamba kikimtililika asijue nini cha kujibu.
Baada ya Stephano kukaa kimya kwa dakika kadhaa bwana yule aliamka na kuongea lugha ambalo hakuiyelewa hata kidogo na sekunde kadhaa alinyanyuka kijana mmoja na kumnyanyua pale chini na kuimuingiza chumbani, chumba ambacho kilikuwa na giza.
Mapigo ya moyo yalidunda kwa haraka huku akijarubu kupepesa macho.
Muda mchache aliingia mtu mmoja na mlango ukafungwa sekunde chache taa kubwa ikawashwa na mwanga ukaenea kwenye kile chumba kwa mbele kulikuwa na viti viwili na meza, Stephano alipogeuza macho mlangoni kwa mara nyingine Stephano anakutana tena na yule baunsa alietoa hukumu kwa kijana ambaye alichomwa kisu huku stephano akishuhudia kwa macho yake.
Stephano kabla ya kuongea kitu chpchote alimuangalia baunsa yule ambaye sura yake na roho yake wala havikuwa na utofauti wowote. alionekana ni mtu mwenye roho mbaya tofauti na watu wote
Baunsa yule hakuongea kitu chochote alitembea mpaka kilipo kiti na kuketi, kisha akavua mawani yake na kuiweka juu ya meza.
Baada ya muda mchache yule baunsa aliongea kwa sauti ya ukali sana
"Sijaingia humu kukutazama kama picha ninamazungumzo na wewe"
Alipomaliza kuongea maneno yale alimuonyesha kwa ushara kuwa akae kwenye kiti ambaocho kilikuwa mbele yake.
Stephano alijongea taratibu na kuketi kwenye kiti na kukaa kimya, alifahamu vizuri kuwa aliyekuwa mbele yake hakuwa mtu wa masihara hata kidogo.
Yule baunsa kabla hajaendelea kuongea aliingiza mkono mfukoni na kutoa sigara na kuiwasha na kupuliza moshi ambao ulimfanya Stephano akohoe.
Kitendo kile cha kukohoa kilimfanya yule baunsa acheke na kuongea
"Nini tatizo ambalo linakufanya ukohoe"
Stephano alinyamaza kimya na yule baunsa akaendelea kuongea.
"Nina maswali manne ukiyajibu ipasavyo naweza kukwambia utakuwa umepona na adhabu zangu.
Stephano alishtuka na kunyamaza kimya baunsa yule alivuta sigara kisha akapuliza moshi mwingi ambao ulimfanya stephano akohoe.
Kabla ya kuuliza swali alisimama na kuweka mguu juu ya kiti na kumuangalia Stephano ambaye muda wote alikuwa akitetemeka
"Naomba unijibu swali langu kama ifuatavyo, kati ya wewe na Anna ni nani ambaye alimtongoza mwenzake?"
Swali lile lilikuwa jepesi sana kwa alieuliza ila lilikuwa gumu kwa anaetakiwa kutoa ajibu Stephano alifikilia kichwani mwake kisha akamtaza ma yule baunsa na kumwambia
"Huyo Anna ambaye unamtaje mimi mbona simfahamu"
Baada ya kuongea maneno yale baunsa alirudia takribani mara tatu lakini stephano alishikilia msimamo wake wa kutomfahamu Anna.
Baada ya kutoridhika na majibu yale alichukua simu yake na kumpigia boss wake na kumueleza, boss wake alitoa kauli moja tu.
"Ninachokitaka ni jibu linalo eleweka na sio maelezo"
Baada ya kujibiwa maneno yale na bosi wake aliwaita vijana wanne ambao waliingia huku mikononi wakiwa wameshika waya za umeme
"Mungu wangu nakuomba unisaidie"
Stephano aliongea maneno yale huku vijana wale wakizidi kusogea eneo lile na sekunde chache mlango ukafungwa. Baunsa ambaye alikuwa anamuhoji Stephano aliongea na vijana wale wanne kwa ishara ambayo Stephano hakuelewana kisha wote wakatikisa vichwa kisha yule baunsa ambaye alikuwa akimuhoji akafungua mlango na kutoka na kuwaacha vijana wale hapo ndipo ambapo Stephano alijionea kwa macho yake kuwa kuna watu wakatili duniani.
*********ITAENDELEA******************
JE NI KITU GANI AMBACHO KINAENDELEA TUKUTANE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba mwendelezo wa hadithi ya stephano nimeishi episode a 13
ReplyDelete