endelea kusoma kisa hiki cha kusisimua


WHY ME_________(03)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia jana.
Frank aliwaza na kuwazua na kumwambia.
"Twende huku tukimkosa na huku basi tutarudi hapahapa kwake"
Waliongozana huku wakiwa wanapiga stori za hapa na pale dakika chache walifika sehemu husika na Anna hakuamini kwa macho yake, baada ya kumkuta stephano kwenye hali inayomfanya Anna atokwe na machozi.
SHUKA NAYO SASA
Alimuona stephano ambaye yupo tofauti na yule aliyemzoea siku zote, kipensi alichokivaa hakikujulikana hata rangi yake kutokana na vumbi la matofali aliyokuwa anayabeba 
"Inamana Stephano hii kazi anayofanya siku zote?"
Frank alicheka na kumwambia
"Stephano yupo tofauti sana na vijana wengine hapa mtaani, unadhani nani atakayemuomba ela ya kununua daftari kila siku wakati hana wazazi, au nani ambaye angeweza kumsaidia kama yeye mwenyewe hajitumi".
"Mh hapana, kweli kila binadamu anaishi kwa style yake"
Baada ya Anna kumaliza kuongea vile Frank alimuita kwa sauti na kugeuka kisha akamjibu kwa sauti
"Nisubiri kama dakika tano nitakuwa nimemaliza"
ilikuwa ni sehemu ambayo kila mtu alionekana kuwa bize Anna akuacha kumuuliza maswali frank ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa Stephano
"Inamana kazi hii kwa siku anaweza akapata kiasi gani"
"Kiukweli nisikudanganye mimi sijui vizuri ungemuuliza stephano mwenyewe"
Muda mchache stephano alimaliza kupakiza matofari kwenye gari wakati anakuja kwa Frank alijiuliza maswali mengi baada ya kumuona Anna
"Inamana huyu mwanamdada bado anaendelea kunifatilia tu"
Sekunde chache alifika na kuwasalimia kwa pamoja na wote waliitikia kisha frank akamuuluza
"Vipi Stephano kuna uhakika wa kufanya mtihani jumatatu?"
"Frank ndugu yangu hapa sielewi hata nifanyeje hii kazi nafanya tu kwakuwa sina jinsi lakini hela hatupewi leo mpaka jumanne"
"Kwahiyo jumatatu mtihani utaukosa"
"Sina jinsi frank ila nakushauri frank, Soma si unaona wazazi wako wanavyohangaika kwa ajili yako, natamani hata mimi ningekuwa nahudumiwa na mzazi wangu nisingepata shida kiasi hiki"
Maneno ambayo aliyaongea Stephano yalimfanya Anna atokwe na machozi mbele ya frank na Stephano mwenye kitendo kilichomfanya Stephano amuulize
"Frank analia nini huyu dada?"
"Huyu dada alikuwa anashida na wewe sasa sijui analia nini inabidi umsikilize kwa umakini"
Stephano alishusha pumzi na kumsogelea kisha kumwambia 
"Nakusikiliza shida yako ambayo imekuleta hapa"
Anna hakuongea kitu zaidi ya kuendelea kutokwa na machozi takribani dakika mbili nzima Stephano akavunja ukimya na kumwambia frank
"Frank unajua haya ni matatizo unadhani akipita mtu ambaye ananifahamu na kumkuta huyu binti analia unadhani atanifikiliaje mimi"
Baada ya stephano kuongea sana na kutaka kuondoka eneo lile ndipo Anna alipofungua mdomo wake na kumwambia
"Stephano mimi ni binadamu kama nitakuwa nimekuchukiza kwa kitendo kilichotokea naomba unisamehe,
"Nishakusamehe ila ungekuwa vizuri zaidi unge niambia kilichokuketa manake likija gari itanibidi niende nikaendelee na kazi"
"Stephano nilikuwa nina mazungumzo marefu sana na wewe na kuhusu muda wako mimi nitakulipa, na ningeomba tungeenda kwako tukakaa tukaongea vizuri hapa sio mahara pake"
Stephano alishtuka na kumuuliza mara mbili mbili
"Tukaongelee kwangu"
"Ndio"
"Hapana kiukweli ni bola ungenitafuta siku nyingine leo itashindikana"
Frank aliingilia kati na kumaambia
"Stephano hebu msikilize huyo dada nimehangaika naye tangu saa nane tunakutafuta wewe, nimeacha kazi zangu nimemsaidia mpaka tumekupata, alikuwa anatokwa na machozi mbele yako unajua alikuwa analia nini?"
Stephano alijibu kwa sauti ya chini
"Hapana"
"Sasa ndo pakwenda kumsikiliza ujue kinachomfanya aliye"
"Ok twende"
Stephano alikubali kishingo upande hakutaka kumdharau frank ambaye alimsaidia baadhi ya mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wake.
Waliongozana wote watatu kuelekea nyumbani kwa Stephano huku wakiwa wanapiga stori za hapa na pale muda mchache waliwasili kwa stephano aliwakaribisha ndani gafla simu ya Frank iliita alipotaza alikuwa ni mama yake alipopokea mama yake alimsisitizia arudi nyumbani haraka alimuangalia Anna na kumwambia.
"Anna naenda nyumbani ila nitarudi muda sio mrefu, Stephano nakuomba msikilize kwa umakini huyu dada"
Frank aliondoka na kumuachia uwanja Anna wakiwa stephano,
Stephano alimuangalia Anna ambaye alionekana kushangazwa sana na magazeti ambayo yamebandikwa chumba kizima, Stephano alimuangalia kisha akamwambia
"Nakusikiliza uniambie kitu ambacho kimekufanya tutoke kule tuje huku"
Anna alikuwa kimya tu Stephano alipomtazama alimuona bado anaendelea kushangaa Stephano alimgusa Anna begani kitendo kikichomfanya Anna ashtuke ndipo stephano alipotambua kuwa Anna alikuwa kwenye dimbwi la mawazo
"Vipi unawaza nini?"
"Hapana nipo sawa?"
"Ok tambua umenitoa kule ukanileta huku nikipi ambacho ulikuwa unataka uniambie"
"Stephano samahani kama nitakuwa nimekukera kwa swali ambalo nitakuuliza, hivi pale unapofanya kazi kwa siku unaingiza shilingi ngapi?"
Stephano alishtuka na kujisemea kimoyomoyo
"Inamana kilichomleta ndo hiki au"
Wakati akiwa anafikilia jinsi ya kujibu, Anna alimkatisha na kumwambia.
"Tuachane na hayo, nimekuja hapa kwa mambo mawili tu, la kwanza ni kukusaidia wewe uweze kurudi shule na jumatatu uweze kufanya mtihani"
Alipomaliza kuongea vile Anna alifungua kipochi chake na kutoa kitita cha pesa na kumkabidhi Stephano ambaye alipokea huku akiwa anatetemeka.
Baada ya kupokea Anna aliendelea kuongea kwa kusema
"Jambo la pili ambalo limenileta hapa ni mapenzi"
Stephano alishtuka na kumwambia
"Nimesikia vibaya au naomba urudie tena"
"Nirudie nini Stephano nimekwambia nakupenda"
Alipomaliza kuongea vile alinyanyuka na kutaka kusogea karibu ya stephano ambaye alikuwa kanyamaza kimya kwa dakika mbili nzima, sekunde chache stephano alimuuliza Anna swali
"Inamana unataka uninunue kimapenzi, ukaona ukija na pesa nitalainika sindio?"
"Apana sio hivyo"
"ila?"
Anna alinyamaza kimya na Stephano aliendelea kuongea
"Sikiliza dada yangu kama msaada wenyewe ndio huwo nipo radhi niitafute pesa kwa jasho langu na nisiwe mtumwa wa mapenzi"
Alizichukua zile pesa na kumrudishia Anna huku akiendelea kuongea
"Pesa sio mapenzi, zinaweza kununua ngono na sio mapenzi, Inamana umekuja kununua ngono kwangu, dada kwa hilo halitowezekana nakuomba uniache nikaendelee na kazi yangu"
"Hapana stephano tambua kuwa sipendezwi na maisha ambayo unaishi maisha ya kufanya kazi ngumu ambazo kipato chake ni kidogo"
"Wewe kama unakiona kidogo mimi kinanitosha hicho hicho nitapataje kipato kikubwa angali bado mwanafunzi"
Anna alipojibiwa vile hakuwa na chakuongeza zaidi ya kukaa kimya, alipogeuka upande wa pili alikiona kisu na alipomuangalia Stephano alikuwa ameinamisha kichwa chini, alikichukua kile kisu na kumwambia
" Stephano chagua moja niwe hai au kupoteza maisha yangu na wewe uwende polisi"
"Stephano alishtuka aliposikia vile na aliponyanyua kichwa alimuona Anna ambaye alikuwa ameshika kisu.
"Anna usifanye hivyo tafadhari, nakuomba weka kisu chini"
Anna alizidi kuongea kwa sauti.
"ukinikubari ndipo nitakapoweza kukishusha kisu kama ukinikataa nipo radhi nife mbele yako na wewe utahusishwa kwenye kesi ya mauwaji"
**********ITAENDELEAA***********
JE STEPHANO ALITOA JIBU GANI KWA ANNA
TUKUTANE SEHEMU YA NNE YA HADITHI YETU YA WHY ME

No comments