gusa apa ili uweze kusoma hadithi hii yenye kisa cha kusisimua


WHY ME_________(04)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia jana.
"Stephano alishtuka aliposikia vile na aliponyanyua kichwa alimuona Anna ambaye alikuwa ameshika kisu.
"Anna usifanye hivyo tafadhari, nakuomba weka kisu chini"
Anna alizidi kuongea kwa sauti.
"ukinikubari ndipo nitakapoweza kukishusha kisu kama ukinikataa nipo radhi nife mbele yako na wewe utahusishwa kwenye kesi ya mauwaji"
SHUKA NAYO SASA
Stephano alishikwa na butwaa na kuwaza mambo mengi kichwani mwake Anna alizidi kuongea huku akizidi kutoa vitisho vikali sana
"Chagua moja kati ya hayo niliyokwambia, Stephano naomba unipe jibu kama sivyo nitachukua uwamuzi mgumu ambao utajutia ndani ya maisha yako"
"Huyu nguvu aliokuja nayo ameipata wapi"
Stephano alijiuliza maswali kichwani mwake bila ya kupata jibu kisha alifungua mdomo wake na kumwambia Anna.
"Kama kweli unaupendo wa thati utanisikiliza ninachokwambia nakuomba shusha kisu chini kama kweli unanipenda na kama ulikuja kwangu kwa lengo la kunitafutia matatizo basi fanya unachotaka kukifanya"
Maneno aliyoyaongea Stephano yalimfanya Anna aendelee kuongea huku akitokwa na machozi
"Moyo wangu unauma sana kuona unaishi maisha haya au unataka mpaka nikwambie kuwa hizo pesa nilizokuketea kuwa nimeuza simu yangu kwa sababu yako"
Stephano alishtuka baada ya kusikia maneno ambayo ameyaongea Anna aliinama chini kisha akanyanyua uso wake na kumwambia
"Anna fahamu fika kuwa wewe ni msichana uzuri wako umekumbana na vishawishi vingi sana vya wanaume je uliwahi kumkubalia mwanaume siku hiyohiyo hata kama ulikuwa unampenda kwa dhati?"
Anna alinyamaza kimya bila kujibu kitu chochote Stephano aliendelea kuongea
"Lengo langu nilikuwa nataka nikupima, tambua moyo hauna mlango kusema ungefunguka nikaona upendo wako kwangu, ila kitendo ulichonionyesha ni kipimo tosha cha upendo na mimi nakupenda pia"
Maneno yale yalimfanya Anna atupe kisu na kuonyesha tabasamu hafifu ambalo liliambatana furaha.
Baada ya Anna kuzidi kuonyesha furaha yake iliyokuwa imejificha Stephano aliinamisha kichwa chini na kukumbuka tukio kama hili liliwahi kutokea akiwa kidato cha kwanza alipojikuta akili na mawazo yake anayahamishia kwa Sauda, Uzuri wake ulimchanganya sana ila hakusita kumwambia ukweli wake uliopo ndani ya moyo wake, majibu aliyopewa na Sauda hakutaka kuyakumbuka hata kidogo.
Akakumbuka siku ambayo aliitwa na headmaster na kupewa onyo kuhusu Sauda tena alimsisitizia na kumwambia
"Ukiendelea na tabia yako nakufukuza shule"
Tangu siku hiyo alianza kuwaogopa wanawake ambao wengiwao walikuwa wanatabia ya kujihusisha kimapenzi na baadhi ya walimu.
Mawazo hayo yalipelekea kumfanya Stephano azidi kuchanganyikiwa zaidi anapotazama hari yake duni ya kiuchumi kula kwake mpaka afanye kazi.
Anna alimshtua Stephano na kumwambia
"Kama nikivyokwambia hii ela nimekuketea ikusaidie kulipa ada na matumizi mengine kikubwa zaidi nataka jumatatu nikuone shule"
Stephano alizidi kujiuliza kimyakimya
Nikisema nizikatae hizi ela itakuwa matatizo mengine"
Aligeuka na kumuangalia kisha akazipokea na kumwambia 
"Asante"
"Hivi ulichokiongea ni cha kweli au ulitaka kuitikia ili kuepusha shari?"
Stephano alijichekesha na kumwambia 
"Nipo serious na nilichokiongea"
Anna baada ya kusikia vile alifurahi na kumwambia 
"Nataka nirudi nyumbani, kabla ya baba hajarudi kutoka kazini, ila nilikuwa naomba kitu kimoja"
Stephano alimsikiliza kwa makini na kumuuliza
"Kitu gani hicho"
"Nataka uniage kwa kunibusu kama kweli unanipenda"
Stephano alifanya kama alivyoambiwa lengo lake Anna aweze kuondoka ndani kwake ili aendelee na mambo yake.
Anna alitoka nje na kumuaga Stephano kisha taratibu akaanza kuondoka. Stephano kwa hasira alinyanyuka kitandani na kupiga teke ndoo ya maji ya kunywa ambayo iligonga kwenye ukuta na kutoa sauti ambayo ilimfanya Anna arudi kwa speed na kumkuta Stephano akiwa ameinama huku anaongea peke yake kama chizi.
Anna alisimama mlangoni na kumya huku Stephano akizdi kuongea 
"Sasa kilichonifanya nimkubalie ni kipi hasa akhaa"
Aliponyanyua macho mbele alikutana uso kwa uso na Anna ambaye alikuwa Amesimama mlangoni akimsikiliza maneno yote aliyokuwa anaoyaongea na kumuuliza
"Kwahyo unataka kubadili maamuzi sindio?"
"Hapana kuna kitu ambacho kinaniumiza kichwa"
"Endelea kuwaza ila unachokiwaza ukibadili maamuzi kitakugharimu"
Alipomaliza kuongea maneno yale aliondoka na kumuacha Stephano akiwa kimya.
Alinyanyuka na kuchungulia nje hakuona mtu alifunga mlango na kuendelea kuongea
"Nitabadirisha maamuzi na chochote afanye, na pesa zake namrudishia kama zilivyo, akiniuliza kwanini nimebadirisha maamuzi namwambia kuwa mimi nimeathirika ili asiwe na nguvu ya kuendelea kunilazimisha"
Akiwa anaendelea kuongea peke yake gafla mlango ukagongwa alishtuka na kusema
"Inamana alikuwa hajaondoka tu, au atakuwa alijificha nyuma"
Mlango ulizidi kugongwa Stephano alinyamaza kimya huku akiwa anahangaika kuchungulia nje, mgongaji baada ya kugonga mlango sana ndipo alipoamua kuongea kwa sauti
"Stephano sinimekusikia ulikuwa unaongea hebu nifungulie"
"Frank?"
"Ndio"
"Nilijua Anna"
Alifungua mlango kisha akachungulia kushoto na kulia akiendelea kuongea na kuzidi kumlaumu frank
"Yule mwanamke wako uliyemleta sitaki nimuone tena hapa"
"Stephano mwanamke wangu tena sio wako?"
"Wewe ndo ulimleta, frank nishazoea kuishi nikiwa na amani muda wote, yule mwanamke alitaka kujichoma kisu ndani kwangu,
Frank alishtuka na kuendelea kumsikiliza stephano
"Kaniachia ela zile pale kitandani wala sijazihesabu na wala sitaki kujua ni kiasi gani nataka nimrudishie mwenyewe"
Frank alishangaa sana kitu alichokiongea stephano na kumwambia
"Stephano sasa uwo ni upumbavu, kwani wewe ulimuomba si amekufata mwenyewe bahati kama hizo hatuzipatagi sisi wajanja, wanazipata wajinga wasiojua kuzitumia"
"Shukrani kwa kuniita mjinga ninavyojua mimi mjinga ni yule ambaye haelewi anachokifanya haujui kuwa hizi ela kazipata wapi na baba yake anafanya kazi gani unaweza ukajikuta unaingia mamtatizoni hivihivi ila ninachokuomba niache na ujinga wangu baki na ujanja wako"
Baada ya maongezi ya muda mrefu frank aliondoka na kumuacha stephano ambaye walipishana kauri kidogo na stephano.
Aliwaza na kuwazua kisha akili ikamcheza na kuzihesabu zile pesa zilikuwa zinapata laki mbili aliziangia zile pesa na kusema
"Kesho ni siku ya mtihani shuleni inamana niukose mtihani kwa sababu ya kudaiwa ada ya shule na pesa ninayo mkononi, hapana nitatumia kiasi cha pesa ambacho nadaiwa shuleni kisha nitazirejesha na kumrudishia mwenyewe, ila nitaweza kweli?"
Alijiuliza mwenyewe huku akiendelea kuzitazama zile pesa kwa umakini wa hali ya juu.
SIKU ILIYOFUATA
Ilikuwa siku ya jumatatu, siku ambayo kila mwanafunzi alijiandaa kikamilifu na mitihani, wanafunzi walisismama asamble wakiwa tayari kuingia madarasani ili kukabiriana vyema na mitihani, Anna aligeuza macho yake kulia na kushoto kumuangalia Stephano bila mafanikio yoyote, Muda mchache headmaster alisimama na kuongea mbele ya wanafunzi na kusema
"Zoezi langu linaendelea kama kawaida kama unajijua haujamaliza kutoa ela ya ada usiingie darasani kwani nikikukuta umeingia darasani utapata adhabu kari sana"
Alipomaliza kuongea maneno yale aliwaruhusu kuingia madarasani, Anna alizidi kupapasa macho huku na kule kwenye umati ule wa wanafunzi hatimaye akapata nafasi ya kumuona frank, alimfata na kumsalimia cha kushangaza frank alimtolea maneno ambayo yalimfanya Anna abaki mdomo wazi.
************ITAENDELEA***********
JE FRANK ALIMJIBU KIPI ANNA, NA STEPHANO ATAKUJA SHULE?"
TUKUTANE KWENYE SEHEMU YA TANO

No comments