SIMULIZI YA KWELI ambayo itakufanya uweze kuburudika

WHY ME_________(02)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia jana...,.
Anna alinyamaza kwa sekunde chache na headmaster alipiga meza kwa hasira na kuongea kwa
ukali hali iliyomfanya Anna kuingiwa na uwoga na kukosa chakuongea, akiwa bado amesimama pale mlangoni headmaster aliongea kwa ukali
" Toka rudi darasania na kesho nitamuita mzazi wako"
SHUKA NAYO SASA.
Anna alitaka kuongea kitu lakini mwalimu alinyanyuka na kuzidi kuongea kwa hasira kitendo kilichomshangaza mwasibu, aliondoka na kurudi darasani huku akiwa mnyonge na kukaa kwenye kiti na kukilaza kichwa chake kwenye meza.
Muda mchache kengere ya kurudi darasani iligongwa na kila mwanafunzi alikimbilia kwenye darsasa lake, sekunde chache mwalimu wa mathematics aliingia darasani huku akiwa amebeba fimbo zake darasa lilikaa kimyaa kwa dakika kadhaa, mwalimu aliwangalia wanafunzi wote na kuongea kwa sauti
"We binti ambaye umelala unaumwa"
Anna alinyanyua uso wake ambao ulikuwa unatokwa na machozi na kumjibu
"Ndio mwalimu kichwa kinaniuma"
"Nenda kwa headmaster kamumbe suspention uwende nyumbani ukapumzike"
Anna alinyanyuka na kuelekea tena kulekule kwa mwasibu na kugonga tena mlango headmaster alipogeuka alitaka kuongea mwasibu akamkatisha na kumwambia
"Mpe nafasi ya kuongea hujui ni kipi ambacho kimemleta kwa mara ya pili, binti
ulikuwa unasemaje?
"Mimi nimetumwa na baba anataka kufahamu stephano anadaiwa kiasi gani cha pesa"
Headmaster alimuuliza Anna huku akimuangalia usoni
"Unauwakika na unachokiongea"
"Ndio"
"Nimpigie simu baba yako nimuulize"
"Ndio mpigie"
Anna alijikuta anajibu bila ya kuogopa kitu chochote na kumfanya headmaster kuamini, Mwasibu hakuchelewa alipekuwa makabrasha yake ipasavyo na kumwambia
"Kamwambie anadaiwa laki na sabini na kama ikifika mwezi wa sita kama hajalipa tutamsimamisha shule mpaka amalize kulipa"
"Asanteni wakuu wa shule anna aliondoka huku akiwa na furaha moyoni mwake na kurudi darasani na kukuta adhabu inaendelea darasani alikaa kwenye kiti chake na mwalimu akamuuliza
"Mbona hauwendi nyumbani?"
"Kwa sasa najisikia afadhari"
Darasa zima lilipata adhabu kasoro Anna ambaye mwalimu alimuonea huruma, baada ya kutoa adhabu mwalimu kuongea kwa hasira
"Inamana darasa zima mumelishindwa hili swali sindio maana yake?"
Mwanafunzi nmoja alinyoisha mkono na kusema
"Mwalimu sio kama tumelishindwa hilo swali ika hiyo topic haujawahi kutufundusha"
Mwalimu alicheka na kuongea
"Shule za serikali sio kila kitu mwalimu akafundishe stephano kila siku lazima aje ofisini, na akija anakuwa kashafanya zoezi kwa kupitia mifano ya kwenye kitabu mimi nasahisha tu. vilevile kama kuna sehemu amekwama anaomba nimsaidie hili swali kwa mtu kama stephano ni sawa na kumsukuma mlevi tu, na kutaka kuamini hili swali nitaluacha kama home work siku atakayokuja tunalifanya wote hapa hapa ubaoni"
Baada ya kumaliza kuongea vile mwalimu alinyanyua kitabu chake na kusema
"Tutaonana ijumaa tutakuja kusolve baadhi ya maswali tukiwa tunajiandaa na mitihani jumatatu"
Kisha akatoweka huku baadhi ya wanafunzi wakaanza kuongea darasani frank ambaye ni rafiki yake mkubwa sana stephano alienda mbele ya darasa na kuongea kwa sauti ya juu huku akiwa anacheka
"Stephano ukimwambia achague kitu ambacho hana katika maisha yake atachagua pesa, sisi darasa zima tutachagua akili ndizo ambazo hatuna"
Baadhi ya wanafunzi sana walicheka sana ila ulikuwa ni ukweli kuwa
Maisha ya Stephano yalikuwa ayaeleweki kabisa dhiki ufukara na kila shida ilikuwa ni sehemu ya maisha yake,
kwa umri wake aliofikia ilikuwa ni bahati sana kwake, akuwahi kuonja malezi ya wazazi wake mama yake alifariki akiwa na wiki mbili tu tangu amlete duniani Stephano.
Stephano alilelewa na bibi yake ambaye naye alifariki dunia na kumwacha Stephano akiwa na darasa la nne, huo ukawa mwanzo wa uyatima kwa Stephano.
Hakumjua baba yake kwa sura ila alimtambua kwa jina ambalo liliandikwa kwenye kadi yake ya krinik, baba yake alimkataa Stephano akiwa bado tumboni kwa mama yake,
Mpaka alipofikia sasa Stephano hakuna kazi ambayo hakuwahi kuifanya aliokota vyuma chakavu, alifyatua matofari alibeba mizigo kwenye Stend ya muheza ila vyote hivyo hakuacha kwenda shule, kitu ambacho hata bibi yake alimsihi sana.
Ilikuwa siku ya ijumaa stephano aliwasiri shuleni majira ya saa nne kamili asubuhi mguu wake aliupeleka moja kwa moja mpaka kwa mwasibu alipofika mlangoni alikutana na headmaster alimuamkia kisha kumwambia
"Mwalimu nimeangaika nimeweza kupata kiasi hiki kidogo cha fedha nilichokuwa naomba jumatatu niweze kufanya hata mitihani"
Headmaster alicheka na kumwambia
"Ubatupangia kazi kama shule ya baba yako"
Stephano alichukia sana kutajiwa mtu ambaye alimkataa na kusema
"Sasa kama shule ingekuwa ya baba yangu ningehangaika kiasi hichi, mwalimu binadamu hatupo sawa kimapato hata kielimu najua wewe umesoma mpaka kufikia hatua hiyo, najua ulijari sana elimu na ulikutana na changamoto tofauti tofauti, maisha yangu ni tofauti na wanafunzi wenzangu wengi wanasomeshwa na wazazi wao ila mimi ndio baba na mimi ndio mama"
Mwalimu akujibu kitu aliondoka na kumuacha pale pale mlangoni stephano hakujali aliingia kwa mwasibu na kukabidhi kiasi kile cha pesa na kutoka nje.
Muda mchache kengere ya mapumziko iligongwa na wanafunzi walitoka nje kumpumzika stephano hakuwa na chakusubiri zaidi ya kuondoka alipopita eneo la darasa lao alisikia sauti ikiwa inaita alipogeuka alikuwa ni frank
"Vipi stephano mbona umekuja na nguo za nyumbani"
"Kuna kiasi kidogo cha pesa nilikileta"
"Kwahyo jumatatu ndani ya pepa kama kawa"
"Sijui kama nitafanya ila nitakuja kujaribu manake headmaster kanitolea nje"
Frank alitikisa kichwa na kumwambia
"Pole sana ndugu yangu ila mimi nitajua jinsi gani ya kufanya mpaka wewe ufanye mtihani"
"Frank nitashukuru kama unayoyaongea yatakuwa kweli ila ngoja niwahi nyumbani kuna kazi nikamalizie kuifanya"
"Haina shida Stephano"
Waliachana huku frank akiwa anawaza juu ya rafiki yake kukosa kufanya jumamatu alipoingia darasani alipata ugeni wa gafla
"Samahani kaka"
"Bila samahani"
"Nilikuona ulikuwa umesimama na stephano vipi anaweza kuja shuleni jumatatu"
"Hapana hicho ndicho kitu ambacho kinanifanya hata mimi nikose raha"
"Mimi nitamsaidia"
Frank alishtuka na kumwambia
"Acha utani kama unachokiongea ni cha kweli basi itakuwa vizuri zaidi"
"Nipo serious"
Frank alimsikiliza kwa umakini na kumuuliza swali
"Kesho jumamosi kama uwakika lazma apate kesho jumamosi au keshokutwa"
"Kitu cha msingi ni wewe ungeniachia namba yako alafu mimi nitakutafuta siku hizo mbili"
Frank alifanya kama alivyoambiwa bila ya kupoteza muda huku Anna akipiga hesabu jinsi ya kuipata pesa ambayo atamsaidia stephano.
SIKU MBILI BAADAYE
Ilikuwa jumapili jioni frank akiwa amejipumzisha alipokea ujumbe mfupi ambao ulitumwa na mwanadada Anna.
"Naomba tuonane jioni ya leo kwa sababu ule mpango umeshakamilika, kinachotakiwa ni kumtafuta stephano leo hii mpaka apatikane"
Frank alinyanyua simu yake na kumpigia na kumwambia
"Tukutane shuleni sasa hivi ili twende nyumbani kwa stephano"
Anna alivyoambiwa maneno yale hakupoteza muda alichukua kipochi chake na kuelekea maeneo ya shuleni, dakika chache frank alifika na kumkuta Anna amekaa akimsubiri yeye.
"Vipi umefika muda mrefu sana"
"Apana kama dakika kumi zilizopita"
"Sawa tunaenda kwa stephano unaenda kumwambia kuwa kesho aje shule au manake nataka nijue kabisa"
Anna alicheka kisha akafungua kipochi chake frank alishtuka kuona burungutu la hela na kumwambia.
"Umezipata wapi hela zote hizo"
"Usijali utafahamu ningeomba tuwahi kwenda kabla baba ajarudi nyumbani"
Safari ikaanza huku Anna akiendelea kumuoji maswali frank ambaye aliyajibu mpaka akaona kero na kumwambia
"Anna maswali mengine utamuhoji muhusika mwenyewe, niliokujibu mimi ndio ambayo nayafahamu"
Dakika chache walifika kwa stephano na kukuta mlango umefungwa.
"Dah hapa ndipo kwa stephano ila kama unavyoona pamefungwa"
"Sasa tunafanyaje?"
Frank aliwaza na kuwazua na kumwambia.
"Twende huku tukimkosa na huku basi tutarudi hapahapa kwake"
Waliongozana huku wakiwa wanapiga stori za hapa na pale dakika chache walifika sehemu husika na Anna hakuamini kwa macho yake, baada ya kumkuta stephano kwenye hali inayomfanya Anna atokwe na machozi.
*********ITAENDELEAA************
JE ANNA ALIMKUTA STEPHANO KWENYE HALI GANI
TUKUTANE SEHEMU YA TATU YA WHY ME.
ONYO
MARUFUKU KUTUMIA KUKOPY WALA KUITUMIA KIVYOVYOTE HADITH HII BILA RIDHAA YA MWANDISHI
ANAEPATIKANA KWA NAMBA
0715293971

1 comment: