WHY ME_________(12)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
Mwalimu akacheka kisha akawaambia wale vijana wawili 
"Jitambulisheni awafahamu"
Kijana mmoja aliingiza mkono kwenye kiuno na kuchomoa bastora na kumwambia
"Hatujaja kupoteza muda wala kubishana na wewe twende kwenye gari"
Walimchukua Stephano na kuingia naye kwenye gari aina ya Noah na gari iliondoka speed huku mwalimu katunzi akiwa anatetemeka kwa uwoga.
SHUKA NAYO SASA
Baada ya tukio lile mwalimu alirudi ofisini haraka huku akiwa anatetemeka, baadhi ya walimu ambao walikuwa ofisini walishangazwa na hali ambayo alikuwa nayo mwalimu katunzi ambaye alijikojolea bila yeye mwenyewe kujua.
Mwalimu Ester alinyanyuka na kumuuliza mwalimu katunzi huku akipepesa macho kushoto na kulia.
"Kuna usalama kweli mwalimu? mbona unatutia mashaka ni kipi ambacho kimetokea"
Mwalimu katunzi alikuwa kama mtu ambaye amechanganyikiwa, kwani alikuwa anatetemeka huku macho yake yakiwa yanaangaza nje.
Kitendo hicho kilimfanya kila mwalimu ambaye alikuwa ofisini amtazame yeye.
Baada ya dakika kama tano kupita mwalimu katunzi alikuwa kwenye hali ya kawaida, aliweza kuelezea namna ya tukio lilivyotoke na jinsi wale vijana walivyojitambulisha kuwa Stephano ni nddugu yao hakuwawekea mashaka.
Walimu wote walistahajabu huku wengine wakishindwa kuamini kilichotokea ndipo mwalimu mmoja akaongea
"Munakumbuka wiki moja iliyopita hapa kijijini lilitokea tukio ambalo kila mwanakijiji lilimuacha mdomo wazi"
Mwalimu ester akadakia maongezi
"Nikweli sasa hivi itatubidi tuishi kwa mashaka sana"
Sospeter akaongea huku akionyesha kuchukizwa na tukio hilo na kuwatoa akili baadhi ya walimu
"Nimekaa kimya kwa muda mrefu sana, Sijaona mwalimu yoyote alietoa ushauri wa kufikisha hizi habari kituo cha polisi, Naomba niwaulize munalichukuliaje hili tukio, Naona munalichukulia kama kiunganishi cha kukumbuka matukio yaliopita tuache upumbavu mwanafunzi kachukuliwa shuleni inapasa shule kwajibike"
Alipomaliza kuongea maneno yale alinyanyuka na 
Walimu ambao walikuwa ofisini wote walinyamaza kimya hakuna mwalimu ambaye aliongea wala kukohoa mpaka Sospeter alipoingia kwenye ofisi ya mkuu wa shule.
Headmaste baada ya kupelekewa taarifa aliomba ipigwe kengere ya dharura na wanafunzi warudishwe nyumbani ili walimu wakae na kujadiri tukio hili
Gari lilitembea kwa speed huku vijana wale wawili wakiendelea kumtolea maneno ya vitisho Stephano. Kitendo ambacho kilizidi kumuogopesha.
Baada ya kufika maeneo ya michungwani gari lilisimama pembezoni mwa barabara na kijana mmoja alitoa simu na kuipiga na kuongea maneno makali
"Boss tumeshamaliza kazi yako tunachokitaka utuandalia pesa yetu keshi" 
Sauti ya yule mtu ambaye aliitwa bosi ilisikika ikicheka na kuongea kwa kujiamini hasa.
"Kijana hiyo kazi niliowapa mbona ni ndogo sana ela yenu mutaipata wala musijali, kinachotakiwa mufanye kama inavyotakiwa kufanya tu na si vinginevyo"
Baada ya kumaliza kuongea maneno yale alikata simu, Stephano aliisikia vizuri sauti ile ya boss wao na haikuwa ngeni masikioni mwake, aliwaangalia vijana wale na kuwaambia huku akiwa analia
"Ni kipi hasa munataka kutoka, tambueni kuwa mpaka hapa nilipo siwafahamu nyinyi ni akina nani?" na muna lengo gani"
"Kijana ambaye alikuwa anaendesha gari alicheka sana na kumwambia
"Dogo wewe tulia mpaka mwisho wa safari utafahamu kinachoendelea"
Alipomaliza kuongea maneno yale alimuangalia mwenzake na kumuonyeshea ishara ambayo hakufahamu ni ishara ya nini.
Baada ya dakika kama mbili Stephano alizibwa na kitambaa puani kila alipojaribu kuvuta pumzi akawa anazidi kuishiwa nguvu hatimaye akavuta madawa ambayo yalikuwa kwenye kile kitambaa na kulala usingizi mzito akiwa mikononi kwa wale vijana wawili.
Baada ya Stephano kupoteza fahamu vijana dereva aliwasha gari na safari ikaendelea huku wakiwa na furaha ya kukamilisha kazi ambayo wamepewa.
Majira ya saa kumi fahamu zilimrejea bado alishangaa bado yupo kwenye gari na gari inaendelea kutembea alishindwa kuvumilia na hatimaye akafungua mdomo wake na kuuliza
"Kwani tuelekea wapi jamani mbona munazidi kunitia wasiwasi ndugu zangu"
Dereva akadakia na kumwambia
"Hapa hakuna ndugu yako hata mmoja tena atutako usumbufu au unataka tufanye kama tulivyokufanyia mara ya kwanza"
Baada ya kusikia maneno yale Stephano akanyama kimya na safari ikaendelea.
Majira ya Saa moja usiku dereva alishuka kwenye gari na aliporudi alirudi na mifuko mitatu ambayo ilikuwa na vyakula ndani yake alimpatia kila mmoja mfuko wake wa chakula na kusisitiza kuwa wale haraka kabla hawajaendelea na Safari.
Kila mtu alikuwa bize kula chakula mwanzoni ila baada ya dakika 5 Stephano alihisi kizungu zungu kabla hajaongea chochote macho yalianza kuwa mazito akajaribu kupambana na ile hali lakini madawa yalimzidi nguvu na usingizi mzito ukamvamia kwa mara ya pili.
Baada ya masaa matatu kupita Stephano alishtuka akiwa kwenye giza nene huku akiwa amevungwa mikono na miguu tena akiwa amevuliwa nguo zote na kubakishwa na bukta tu.
Alishtuka na kuanza kugeuza shingo huku na kule gafla alisikia sauti nzito ikitokea nyuma yake.
"Unashida gani kijana mbona unahangaika"
Kabla ya kujibu chochote taa zikawashwa alipogeuka nyuma alikutana na pande la mtu lenye miraba mnne tena akiwa ameshika bunduki, 
Mapigo ya moyo yalienda mbio alizidi kutetemeka.
Akiwa bado hajui cha kufanya alisikia sauti ikiendelea kuongea 
"Uwezi kulala hapa kama kwa baba yako"
Alipomaliza kuongea maneno yale alitoweka na dakika chache alirudi na ndoo ya maji ya baridi na kumwagia Stephano ambaye alikuwa amelazwa kwenye sakafu. Stephano akaanza kutetemeka baridi huku yule aliemwagia maji akiwa anacheka kwa sauti ya juu.
Kisha akamfata mpaka pale alipo na kumwambia
"Kijana umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana, nyumba hii ukiingia basi usahau kabisa kama utatoka mzima"
Alipomaliza kuongea maneno yale alinyanyuka na kumpiga Stephano teke kali ambalo lilitua moja kwa moja kwenye mbavu za Stephano, Stephano aliongea huku akiwa anaugulia maumivu makali.
"Kwani ni kipi hasa ambacho nimekosa, kipi ambacho kimenifanya niwe hapa nikitumikia adhabu hii, adhabu ambayo hata sielewi chanzo chake"
Kabla hajamaliza kuongea maneno yale taa ilizimwa na giza likatanda tena ukimya nao ukatawala kwenye jumba lile ambalo alikuwa stephano Usiku ule ulikuwa mgumu sana kupata usingizi baridi lilikuwa kali huku mbu nao wakizidi kumshambulia.
Majira ya saa moja asubuhi alitolewa kwenye chumba kijana mmoja huku akiwa amelowa damu mwili mzima kitendo kile cha kutapakaa damu kilishindwa kutambua hata nguo alizovaa zilikuwa ni za rangi gani.
Sekunde kadhaa walikuja vijana watatu ambao walikuwa wamejazia na mmoja wa kijana yule aliongea kwa sauti ya ukali.
"Sina muda wa kupoteza naomba uniambie ukweli"
"Munataka niwaambie ukweli gani?, ukweli ni ule ambao niliwaeleza jana"
Kijana yule ambaye alikuwa anaongea huku akiwa anasua sua mwili wake ulionrkana wazi wazi kuwa ulikuwa umechoka kwa suruba kali za vijana wale..
Mmoja wa kijana yule alirusha teke kali ambalo lilimpata kijana yule, baada ya mabishano ya hapa na pale alitoa amri kuwa auwawe maneno yale yalimshtua stephano ambaye alikuwa analishuhudia tukio lile kwa macho yake.
Kijana mwingine baada ya kupewa kazi na mkubwa wake alichomoa kisu na kumchoma tumboni.
,Bila kuhadithiwa aliona kwa macho yake baada ya sekunde chache yule ambaye alitoa ruhusa ya ku uwawa kijana yule alitembea taratibu kuja kwa Stephano ambaye alikuwa amefungwa mikono na miguu.
Stephano alianza kutetemeka huku akizidi kumuomba mungu na kukumbuka maneno ambayo aliambiwa usiku wa jana.
"Kijana umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana, nyumba hii ukiingia basi usahau kabisa kama utatoka mzima"
Maneno yale na tukio lile vikamfanya azidi kuchanganyikia.
******************ITAENDELEA*****************
STEPHANO YUPO KWENYE MATATIZO MAKUBWA. CHANZO CHA MATATIZO YOTE CHANZO NI NINI?
TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA TATU YA SIMULIZI HII

No comments