WHY ME_________(11)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
"Inavyoonekana baba yake Anna ni katiri"
Stephano alimnyooshea mkono na kumwambia
"Yule kwa jinsi anavyoonekana anaweza kukukata hata sikio na akalitafuna mbele yako"
Wote wakacheka kwa Sauti ya chini, wakiwa katikati ya maongezi gafla walisikia vishindo nje ya nyumba wakanyamaza kimya na sekunde chache mlango ukagongwa.
SHUKA NAYO SASA
Mlango uliendelea kugongwa huku mgongaji akionekana ni mtu wa gadhabu kubwa kwa jinsi anavyougonga ule mlango. Frank alimtazama stephano ambaye alionekana akiwa kwenye wasiwasi mkubwa sana.
Mlango ulizidi kugongwa tena safari hii mgongaji alitumia nguvu tofauti na mara ya kwanza.
Frank alinyanyuka Stephano akamvuta shati na kumuuliza kwa sauti ya chini
"Usiende kufungua anavyoonekana sio mtu mwema hata kidogo"
Frank alitamani amfahamu mtu ambaye anagonga mlango ila alimuangalia Stephano ambaye yupo kwenye matatizo akashusha pumzi na kukaa kitandani na yeye.
Baada ya ukimya wa dakika kadhaa walisikia vishindo vikiondoka eneo lile, Stephano alijisogeza dirishani na kuchungulia kiwizi wizi kwa mbali aliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti meusi wakitoweka.
"Wale ni wakina nani"
Alijiuliza swali hilo bila kupata jibu na kubaki kwenye sintofahamu na maswali kichwani mwake.
Alirudi na kuketi kitandani na kuweka mikono kichwani kama mtu ambaye amechanganyikiwa sekunde chache baadaye alifumbua mdomo wake na kumambia frank kwa sauti ya chini.
"Nilichokiona hakifai hata kuelezea"
Frank alishtuka na kumuuliza huku akiwa na wasiwasi.
"Umeona nini? Stephano"
Stephano alikaa kimya kwa sekunde kadhaa na kumwambia
"Msako bado unaendelea"
"Khaaa! mbona sikuelewi"
"Usichokielewa ni kipi frank, mimi bado wanted"
Frank aliweka mikono kichwani na kumwambia.
"Unauwakika na unachokiongea?"
"Frank mimi nina uhakika na hapa hapanifai hata kidogo inabidi niondoke"
Frank hakukubaliana na uwamuzi wa Stephano hata kidogo na kumwambia
"Sasa unataka uwondoke uwende wapi?"
"Frank tambua kuwa hili tatizo ni kubwa usije ukajikuta unaingia matatizoni mimi najua nakwenda wapi"
Frank alinyamaza kwa sekunde chache na kumwambia"
"Sasa unataka utoke hapo nje unauhakika kuwa akuna mtu"
"Frank hapa nacheza kama kamari kuna kupata na kukosa sina jinsi"
"Sijakuelewa kamari kivipi?"
"Natoka nikikamatwa sawa nisipokamatwa sawa"
"Inamana unajitoa sadaka?"
"Ndio frank ukiamua kufanya jambo usiwe na maamuzi mawili, inatakiwa uwamuwe kitu kimoja"
Alipomaliza kuongea maneno yale alisimama wima na kumtazama frank kisha akamwambia
"Sekunde chache zinazokuja lolote linaweza kutokea"
Frank alinyamaza kimya huku akizidi kumuomba mungu. Stephano alifungua mlango kwa kujiamini na kutoka nje bila hofu yoyote aliangaza huku na kule na kuongea kwa sauti ya chini.
"Funga mlango mimi ndo naondoka"
Frank alifunga mlango na kumuacha Stephano akitoweka usiku ule huku asije anakwenda wapi.
Alitembea huku akiwa na wasiwasi. aliamua kufunga safari usiku ule na kuelekea shambani huko ndipo kungeweza kuwa na usalama angalau wa hasilimia chache, Alipofika barabarani aliona gari aina ya Noah imepaki pembeni hakujari wala kuwaza aliendelea na safari yake ya kuhamisha makazi yake kwa usiku ule.
Majira ya Saa nane usiku Anna alishikwa na haja ndogo aliamka na kwenda kujisaidia ila alishitushwa na kelele za kilio ambacho alikuwa anakisikia kupitia dirisha, alinyemelea mpaka dirishani na kuchungulia nje aliona vijana wanne wakiwa wamevaa makoti marefu mikono yao ikiwa imeshika mapanga, pembeni kulikuwa na mtu ambaye alikuwa amelala chini huku akiwa analia, baba yake akiwa amesimama karibu naye huku akiwa anaongea maneno ambayo hakuweza kuyasikia kwa haraka, Sekunde chache kijana mmoja alifika na kumnyanyua juu yule mtu ambaye alikuwa amelala chini na kumuingiza ndani ya gari. Anna alipozidi kusikiliza kwa umakini ndipo alipogundua kuwa sauti ile ilikuwa ya Masunga.
Mapigo ya moyo yakaenda kasi na kushindwa kuamini kile ambacho anakiona mbele yake.
Alizidi kujiuliza maswali mengi sana juu ya tukio ambalo lipo mbele yake, akakumbuka na maneno ya masunga ambayo alimwambia baba yake mchana akashindwa kabisa kuelewa ni kipi ambacho kinaendelea.
Gafla vijana wale wanne waliingia ndani ya gari na gari likatoka nje ya nyumba ya mzee tony 
"Sasa wanampeleka wapi na mbona wamemfunga kamba mikononi"
Anna alitamani atoke nje ili afahamu kitu ambacho kinaendelea ila alipokumbuka kuwa yeye ndio chanzo cha matatizo ambayo yalimpelekea kufukuzwa kazi masunga alishusha pumzi na kubaki palepale dirishani akichungulia.
Baada ya gari kutoka nje mzee tony alifunga geti na kurudi ndani kulala.
Asubuhi stori ambazo zilikuwa zimetapakaa kijijini ni za Masunga kukutwa akiwa amefariki pembezoni mwa barabara ya kuelekea mafere.
Tukio hilo liliwashtua watu wengi sana pale kijijini, Frank alianza kuingiwa na uwoga huku akiofia usalama wa rafiki yake aliondoka mpaka nyumbani kwa stephano na kukuta kufuri likiwa linabembea mlangoni. Aliondoka na kurudi nyumbani huku uso wake ukiwa na huzuni.
Alifika nyumbani kwao huku akili yake ikiwa bado haipo sawa akaiyanzisha safari nyingine ya kwenda shamba kwa stephano. ilimchukua takribani dakika kumi na tano kufika shambani, alizunguka huku na kule bila mafanikio yoyote, wakati akiwa anahangaika Stephano alimuona vyema kwani alikuwa amepanda juu ya mfenesi huku akipiga dira
Akiwa amekata tamaa kabisa aliamua kurudi nyumbani, akiwa anaondoka alisikia mruzi ambao ulipigwa mara moja tu, na alipogeuka nyuma hakuona kitu akapiga hatua moja mruzi ukapigwa tena na alipoangaza upande wa kushoto alionana uso kwa uso na rafiki yake stephano.
Frank alifika mpaka kwenye mfenesi na kukaa chini na Stephano alitelemka chini, baada ya maongezi mafupi yaliyotawaliwa na salamu frank aliongea kwa masikitiko makubwa sana
"Stephano rafiki yangu hali ya kijijini sio salama Mzee masunga amekutwa amefariki huku maiti yake ikiwa imekatwa katwa mapanga"
Stephano alishtuka na kuongea kwa sauti.
"Unasema nini wewe inamaana unataka kuniambia kha!!"
Alishindwa kuongea na kubaki ameshika kichwa frank akaendelea kuongea kwa unyonge.
"Stephano maisha ambayo unaishi hayana tofauti na mkimbizi, tena naweza kusema heli hata ya mkimbizi kwani anajua anapokimbilia, nakuonea huruma sana unaishi kama popo lala yako juu ya miti shinda yako juu ya miti ni bora urudi kijijini kuliko huku polini ikitokea umepata tatizo hakuna msaada wa haraka"
Stephano alinyamaza kwa dakika chache na kumwambia
"Ni kweli frank ila tambua hili tatizo ambalo lipo kwangu sio dogo kama waliweza kuja polisi basi hata wagambo hawawezi kushindwa kunitafuta"
Frank alinyamaza kwa sekunde chache na kumuuliza
"Inamaana utakaa huku mpaka lini?, mi naona bora kurudi kijijini kuliko kukaa huku shambani"
Stephano alinyamaza kwa sekunde chache kisha akamwambia
"Najua haunitakii mema, wewe mwenyewe umekuwa shuhuda juu ya tukio la jana kwani kila ulipokuwa unapita watu walikuwa wanakuuliza habari zangu frank hapana naomba niache"
Stephano alikataa katakata maneno ambayo aliambiwa na frank.
Frank hakuwa na kingine zaidi ya kumuaga na kurudi nyumbani huku akiuwangalia vizuri ule msitu ambao analala Stephano alikosa furaha kabisa kwani ulikuwa msitu mkubwa ambao umezungukwa na miti mingi na mapoli yakutisha.
BAADA YA WIKI MOJA BAADAYE
Kijiji kilisahau tukio ambalo lilitokea siku za nyuma kila mtu aliendelea na shughuli zake, shule nazo zikafunguliwa wanafunzi wakarudi shuleni baada ya mapumziko ya wiki moja Stephano ambaye alikula sikukuu akiwa shambani alilejea nyumbani akiwa na lengo la kurudi shule ili aendelee na masomo.
Siku iliyofuata aliamka asubuhi na kuvaa nguo zake za shule kuelekea shuleni, alikutana na baadhi ya wanafunzi wenzake na kujiunga nao, kabla ya kuingia madarasani Frank alimuita Stephano pembeni na kumwambia
"Nimefurahi kukuona ukiwa salama rafiki yangu, kubwa ambalo nimekuitia hapa ni kukwambia kuwa baadhi ya mitihani yako ninayo mimi ila huwo mtihani wa mathematic umepiga ''A" darasa zima umelitupa chini"
Stephano alitabasam na kumwambia 
"Frank elimu ndio ufunguo wa maisha kinachotakiwa tupambane ili elimu isituache"
Frank alicheka na kumwambia
"Ni kweli unachokiongea lakini leo siku ya tatu tangu shule ifunguliwe sijaonana na Anna na kila nikipiga simu yake haipatikani"
Stephano alishangaa na kumwambia
"Inamana haujifunzi kupitia tukio langu unataka na wewe yakukute sindio? Frank ukitaka mimi na wewe urafiki wetu ufe taja jina la Anna"
Baada ya kumaliza kuongea maneno yale alitoweka eneo lile na kumuacha frank.
Muda mchache baadaye kengere ya mstarini ikagongwa wanafunzi wakakusanyika asamble na kuingia madarasani.
Baadhi ya wanafunzi walikuwa wapo bize na kujisomea huku wengine wakipiga kelele gafla walishtushwa baada ya kuja mwalimu katunzi na kuongea kwa sauti ya ukali
"Namuomba stephano mara moja"
Mwalimu katunzi baada ya kuongea maneno yale alisimama nje na kumsubiri, Stephano alopotoka nje ya darasa alikutana vijana wawili ambao walikuwa wamevalia suti za garama, Alishtuka baada ya kuwaona wale vijana kabla hajaongea chochote mwalimu katunzi akayatawala maongezi na kuongea 
"Stephano hawa vijana ambao wapo mbele yako walikuwa na maongezi na wewe"
Vijana wale wakatikisa vichwa kisha mmoja akaongea kwa kujiamini zaidi
"Ingekuwa vizuri tungesogea pale kwenye ile gari manake tunataka kuongea faragha kidogo"
Stephano akavunja ukimya na kuwauliza
"Nyinyi ni wakina nani ?"
Swali lile lilimfanya mwalimu wake Stephano kumuangalia na kumwambia
"Hivi unayo akili kweli wewe"
"Samahani mwalimu wao wananifahamu ila mimi bado hizi sura sijawahi kuziona hapa kijijini hivyo nina haki ya kufshamu"
Mwalimu akacheka kisha akawaambia wale vijana wawili 
"Jigambulisheni awafahamu"
Kijana mmoja aliingiza mkono kwenye kiuno na kuchomoa bastora na kumwambia
"Hatujaja kupoteza muda wala kubishana na wewe twende kwenye gari"
Walimchukua Stephano na kuingia naye kwenye gari aina ya Noah na gari iliondoka speed huku mwalimu katunzi akiwa anatetemeka kwa uwoga.
*****************ITAENDELEA******************
JE WALE NI WAKINA NANI NA WANAMPELEKA WAPI STEPHANO?
TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA MBILI YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA

No comments