WHY ME_________(10)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
lakini hakuna kitu alichoweza kusikia. Wakiwa bado wapo kwenye mazungumzo gafla Anna alifika eneo lile huku akiwa anahema kwa na kumnyooshea kidole baba yake na kuongea maneno makali.
Maneno yake yalimshangaza kila mtu,
Aliongea maneno yale huku akiwa anapiga kelele kitendo kilichomshangaza mwenyekiti wa kijiji, kelele zile zikaita majirani.
SHUKA NAYO SASA
Baada ya sekunde chache majirani walijaa eneo lile huku Anna akiendelea kutoa maneno makali ambayo yalimkasirisha baba yake ambaye alikuwa ameinamisha kichwa chini.
Kila mtu aliefika eneo lile alishangazwa na binti yule ambaye alikuwa akitoa maneno makali, kitendo kilichopelekea Mzee tonny ashikwe na hasira na kumsogelea Anna na kumnasa kibao cha nguvu tukio lile lilimuogopesha Stephano ambaye aliona kwa macho yake Anna alivyodondoka chini, Kitendo kile alichokifanya Mzee tonny kiliwashangaza watu wengi sana ambao walifika eneo lile huku wakiwa bado hawafahamu kinachoendelea.
Polisi mmoja akaongea kwa hasira huku akiwa anamfokea Mzee tonny kana kwamba yeye ndo mtuhumiwa
"Unajichukulia sheria mkononi , Afande mfunge pingu atakwenda kutoa maelezo kituoni"
Wakati hayo yote yakifanyika Anna halikuwa analia kutokana na kibao alichopigwa na baba yake, Afande mudi alimshika mkono Anna na kuzunguka naye nyuma ya nyumba na kumwambia
"Samahani binti na pole kwa yaliokukuta, nilikua naomba unisaidie kitu, ningependa nifahamu yule ambaye amekupiga ni nani yako?"
Anna alifuta machozi ambayo yalikuwa yanamchirizika mashavuni kisha akajiweka sawa kwa kukohoa na kuongea huku Afande mudi akiwa anamsikiliza kwa umakini.
"Yule ni baba yangu mzazi, na kitendo kilichoniuma zaidi mpaka mimi kufika eneo hili ni baada ya kupata taarifa kuwa ameenda kuchukua polisi waje kumkamata kijana ambaye anaishi nyumba hii sijajua kosa lake ni lipi"
Afande mudi alimuangalia kwa umakini binti yule ambaye alikuwa anatoa maelezo na kumuuliza swali ambalo Anna hakufikiria kama angeweza kuulizwa swali kama lile,
"Inavyoonekana unampenda sana mpenzi wako na ndomana ulivyopata taarifa ukaja mapema sindio?"
"Hapana sio mpenzi wangu"
"Ila ni nani yako"
"Mwanafunzi mwenzangu?"
Baada ya kujibiwa vile alimpa mkono na kumwambia 
"Asante kwa maelezo yako na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi endapo kama tutahitaji ushirikiano wako tutakupa taarifa"
Afande mudi alliagana na yule binti na kurejea kwa askari wenzake na akahamuru warudi kituoni, Afande mudi alimshika mkono mwenyekiti wa kijiji na kuongea naye faragha kisha akatoweka na kumuacha na wanakijiji wa pale.
Baadhi ya wanakijiji walipata nafasi ya kumuhoji mwenyekiti huku wengine wakijiuliza maswali vichwani mwao 
Baada ya kuona polisi wameondoka na yeye aliondoka eneo lile na kuelekea nyumbani.
Walilifikia gari ambalo walikuwa wamelipaki barabarani Mzee Tonny kabla ya kupanda kwenye gari alimtazama polisi aliyekuwa karibu yake na kumwambia 
"Kwani kosa langu ni lipi hasa, kumuonya binti yangu ndo limekuwa tatizo"
Afande mudi alicheka na kumwambia
"Kosa lako siyo hilo tu mbona binti yako ameniambia ukweli wote"
Mzee tonny alishtuka baada ya kuambiwa maneno yale.
"Ni ukweli gani huo ambao mimi siufahamu?"
"Utakwenda kufahamu ukifika kituoni"
Afande mudi alipomaliza kuongea maneno yale alimuangalia na kuongea kwa ukali ambao hata mzee tonny aliogopa
"Mzee hatujaja kupoteza muda sawa ningeomba upande juu ya gari twende kituoni"
Mzee tonny bila kupoteza muda akafanya kama alivyoambiwa na polisi wakadandika gari yao na Safari ikaanza.
Gari lilipita kijiji kimoja na kupaki pembezoni mwa barabara afande Mudi akatoa agizo kuwa wamfungue pingu na wamuachie huru, Polisi waliokuwepo nyuma ya gari lile la polisi walifanya kama walivyoambiwa kabla hajashuka kwenye gari mzee tonny alisikia sauti ya afande mudi ikisema
"Nina mazungumzo na wewe kiongozi, naomba njoo huku mbele ya gari"
Mzee tonny alitelemka kwenye gari la polisi na kwenda kwa afande mudi, Afande mudi alikaa kimya kwa sekunde kadhaa na kumwambia
"Siku zote sheria ni msumeno huwa unakata mbele na nyuma na haki ipo kwa kila mwanadamu, Tungeonekana wazembe sana kwa kitendo cha kumpiga yule binti mbele ya polisi na tungekuacha bila kuchukua hatua yoyote wale ambao wamekuona kwa macho yao wangesemaje?"
Mzee tonny alinyamaza kimya kisha afande mudi akaendelea kuongea binti yako ameniambia ukweli wote ila nitaufanyia kazi kimya kimya na kama nitabaini alichokisema binti yako basi wewe uyakuwa unamakosa tena utakuwa unahitaji sheria ifate mkondo wake.
Baada ya kumaliza kuongea maneno yale afande aliendelea kumsisitiza kuwa ataendelea na uchunguzi wa kimya kimya hivyo yeye akapumzike nyumbani.
Alifika nyumbani kwao akiwa mnyonge sana kabla ya kugonga geti aliamua kukaa chini huku akiwa hana amani kabisa ndani ya moyo wake, akikkumbuka kuwa yeye ndiyo chanzo cha matatizo yote akajikuta anatokwa na machozi huku akiongea
"Nilihaidi kukusaidia, Msaada wangu umekuwa ni matatizo makubwa sana, sijui watu watakufikiliaje hapa kijijini, haukuwai kuiba wala kudhurumu mali ya mtu, nisamehe bure Stephano kwa kukuchafulia jina lako, nadhani kila mtu atakuwa na maswali mengi kichwani mwake Naomba unisamehe"
Aliendelea kulia huku akijutia nafsi yake kwa kumuingiza kwenye matatizo Stephano ambaye hakuwa na hatiya.
Mzee tonny alikuwa anaongea peke yake njia nzima kama chizi, alikuwa na gadhabu kubwa ambayo ilionekana dhahiri kwenye uso wake.
Alipofika getini alimkuta Anna akiwa amekaa chini huku uso wake ameinamisha chini alimuangalia kwa hasira na kugonga geti, kitendo kile cha Mzee tonny kugonga geti kikamshtua Anna ambaye alikuwa amekaa pembeni ya geti sekunde chache Bwana masunga alifungua geti na Mzee tonny aliongea neno moja tu
"Ingia ndani"
Maneno yale yalimshangaza bwana masunga kwani hakujua kuwa boss wake anaongea na nani, Sekunde chache Anna aliingia ndani hapo ndipo Masunga alipoweka mikono kichwani kwa mshangao Mzee tonny alimuangalia Masunga kisha akamsogelea Anna na kumfyatua teke kali ambalo lilimfanya Anna akimbie ndani na kumuacha Masunga akiwa ameweka mikono kichwani kwa mshangao.
Aliangaza kulia na kushoto akachukua kirungu ambacho anakitumia Masunga kisha akakiangalia na kusema
"Nilikuonya mara kadhaa kuhusu kuwa makini hapa getini ila bado unaonekana kuwa haupo makini, sasa basi nataka nikwambie kuwa nina vijana wengi sana ambao nikiwaleta hapa watafanya kazi kwa umakini wa hali ya juu, Kuanzia sasa hauna kazi tena hapa nyumbani kwangu"
Bwana masunga aliomba msamaha kwa mzee tonny ambaye alionekana kuwa na hasira sana, lakini msimamo wa Mzee yule ulikuwa ni uleule alimuomba akachukue kila kitu chake ili aweze kuondoka ila bado aliendelea kuomba msamaha huku akiwa analia
"Jaribu kunipa nafasi ya mwisho nakuahidi sitarudia tena"
Mzee tonny alimuangalia kwa hasira na kumwambia
"Kama yule kinyago unashindwa kumdhibiti asitoke nje wakija waharifu utaweza kweli?"
Mzee masunga aliendelea kuomba msamaha lakini ilikuwa ni sawa na kazi bure.
Wakati hayo yote yakiwa yanaendelea Anna alikuwa anaugulia maumivu chumbani kwake huku akisikilia vilivyo sauti ya masunga anavyojaribu kuomba msamaha.
Masunga alinyanyuka na kwenda kuchukua begi lake la nguo huku akijaribu kumsihi boss wake amsamehe ila bado alisimamisha msimamo wake.
Alipofika getini mzee tony alimuuliza
"Unadeni lolote ambalo unanidai?
Masunga alitikisa kichwa na kumwambia 
"Umenifukuza ila tambua siri zako ni mimi ambaye nakutunzia na nilazima niziweke hadharani kama unyama unyamani tu"
Alipomaliza kuongea maneno yale alifungua geti na kutoka nje, Anna aliyasikia vizuri maneno ya Masunga na alimuona kwa macho yake baba yake alivyokuwa ameduwaa kwa dakika kadhaa na asijue nini cha kufanya.
Anna alitikisa kichwa huku akisema
"Ni lazima nizijue hiyo siri ambayo masunga anazifahamu.
Majira ya saa mbili na nusu Frank akiwa yupo chumbani kwake gafla mlango ukagongwa alipofungua alikuwa ni Stephano Frank kama kawaida yake alianza kucheka na kumwambia
"Nilizani wamekubeba, nilikuwa najiandaa kesho nikuletee uji kituoni"
Stephano alimuangalia na kumwambia
"Unacheka na kuongea maneno hayo kwa sababu hayajakukuta wewe"
Frank akamkaribisha Stephano ndani wakaketi pamoja na Stephano akaanza kumsimulia tukio zima alivyoliona akiwa juu ya mnazi Frank alishangaa sana na kumwambia
"Inavyoonekana baba yake Anna ni katiri"
Stephano alimnyooshea mkono na kumwambia
"Yule kwa jinsi anavyoonekana anaweza kukukata hata sikio na akalitafuna mbele yako"
Wote wakacheka kwa Sauti ya chini, wakiwa katikati ya maongezi gafla walisikia vishindo nje ya nyumba wakanyamaza kimya na sekunde chache mlango ukagongwa.
***********ITAENDELEA************
JE NI NANI AMBAYE ANAGONGA MLANGO NA BWANA MASUNGA AMEFUKUZWA HUKU AKIWEKA AHADI YA KUTOA SIRI ZOTE ZA MULE NDANI JE NI SIRI GANI HIZO 
ANNA NAYE ANATAKA AZIFAHAMU HIZO SIRI
TUKUTANE SEHEMU INAYOFUATA

No comments