WHY ME_________(09)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
Stephano hakujibu kitu chochote aliondoka na kuelekea balabalani kabla hajaivuka balabala mama ambaye alimchotea maji masaa machache yaliopita akamuita ili ampatie pesa yake kitendo cha kwenda kwa yule mama gari la polisi likasimama maeneo yaleyale Stephano akaliona kwa macho yake.

SHUKA NAYO SASA
Mama mwanakombo aliingia ndani kwenda kuchukua hela ili ampe 
Stephano 
Cha kushangaza baada ya kutoka nje Stephano alishatoweka eneo lile, huku baadhi ya watu ambao walikuwa wamekaa kwenye vijiwe wakiwa wanakimbia ovyo wakati polisi wale wakiwa hawana kabisa hata mpango nao, mama Mwanakombo alifurahishwa sana na baadhi ya wanakijiji waliokuwa wanakimbia, ndipo alipoongea huku akiwa anacheka
"Kinachowafanya mukimbie ni kipi hasa, mtakuja kuvunja miguu bila sababu yoyote, hata Stephano naye amekimbia, mh makubwa"
Aliongea maneno yale huku akionekana kuwa na mshangao ambao ulimfanya abaki kasimama palepale balazani
Stephano alikuwa anatembea haraka haraka huku akiwa na wasi wasi hakuwa na chakufanya zaidi ya kwenda nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa na maswali mengi ambayo yalikosa majibu
"Inamana wananitafuta mimi ninakosa gani hasa? au wamekuja kumsaka yule jamaa ambaye alimjeruhi mkewe na mtoto"
Kila swali alilojiuliza kichwani mwake halikuwa na jibu sahihi.
Alifika nyumbani kwake huku akiwa hana uwakika kama ni yeye ambaye anatafutwa
Aliwaza na kuwazua kisha akatikisa kichwa na kusema
"Kabla haujachukua maamuzi ni lazima ufanye uchunguzi"
Aliangaza kulia na kushoto hakukua na mtu yoyote, alitafuta 
sehemu ya kujificha aliwaza akimbie 
shambani kwakwe, shamba ambalo aliachiwa na marehemu bibi yake.
"Ila nikikimbilia shambani nitajuaje kama ni mimi ambaye natafutwa"
Aliongea huku akiwa anajiamni, aliangaza huku na kule, pembezoni mwa uwanja kulikuwa na mnazi mrefu ambao umejitenga pembezoni mwa nyumba ile, aliangaza huku na kule kwa umakini wa hali ya juu hakukuwa na mtu ambaye alimuona akapanda juu ya mnazi na kukaa kimya.
Baada ya ukimya mingi polisi mmoja akamuuliza mzee tony
"Huyo kijana anaishi nyumba ipi?"
Mzee tonny aliongea huku akiwa anasua sua
"Kwa kweli sifahamu lakini hiki ndicho kijiji anachoishi"
Baada ya mzee tony kuongea vile baadhi ya polisi walichukizwa na mmoja akaonyesha hasira zake nje nje na kuongea kwa sauti
"Sasa unadhani tutampata vipi wakati anapoishi haupafahamu"
Baadhi ya polisi walikaa kimya ndipo afande mudi akatoa wazo ambalo kila mtu alikubariana nalo
"Munaonaje tukitumia ile picha kama mutakuwa mumekuja nayo?"
Wote wakalikubariana ila afande mabura alikohoa na kuongea kwa Sauti ya juu
"Wazo lako sio baya sana ila mipango yako ndo imeferi, ukiangalia raia wote wamekimbia sasa utamuuliza nani?"
Kweli Kijiji kilitulia kwa sekunde chache
Polisi waliingiwa na mashaka huku baadhi ya watu wakiwa wamejificha kwenye kuta za nyumba huku nyuso zao zikiwa zimetokeza nje.
Afande mudi akili ikamcheza kwa mara nyingine akafungua mdomo wake na kuongea
"Unajua kuna kitu nimekumbuka, swala kama hili ukisema umshilikishe mwananchi hata kama mtuhumiwa atakuwa ndani kwake hawezi kukusaidia kwa haraka lazima atasema hamfahamu, ningependa niwashauri kitu.
Polisi wote walitega masikio yao kwa umakini wa hali ya juu, kisha afande mudi akaendelea kuongea
"Ingekuwa vizuri zaidi tungempata mjumbe au mwenyekiti wa kijiji mmoja wapo tungempata ingekuwa vizuri zaidi.
Watu wote ambao walikuwa wanamsikiliza afande mudi walikubali mmoja wa polisi wale akaibuka na swali ambalo lilowafanya wakune vichwa
"Sawa ila ni nani ambaye utamuuliza kwa mjumbe au mwenyekiti, mfano mumeuwona kwa macho yenu mumefika wote wamekimbia na wengine wanachungulia kwenye pembe za nyumba utampata nani ambaye utamuuliza kwa mjumbe"
Polisi wote walinyamaza kimya.
Mzee tony aliangaza huku na kule hatimaye akamuona mama ambaye alikuwa amesimama kwa muda mrefu sana akiwatazama, alimshtua polisi mmoja na kumwambia
"Munaonaje tukienda kumuuliza yule mama"
Afande mudi akamjibu
"Tena ingekuwa vizuri ungeenda wewe ambaye umevaa nguo za kiraia"
Mzee Tony hakupoteza muda akafanya kama alivyoambiwa na afande mudi.
Baada ya mazungumzo machache ambayo yaliambatana na salamu na yule mama akaitoa ile picha na kumuuliza kama anamfahamu kijana yule.
Mama mwanakombo alishtuka baada ya kuiyona ile picha uso wake uliingiwa na uwoga na kusema
"Hapana simfahamu kwani amefanya nini?"
Alitoa jibu lenye swali ndani yake lakini Mzee Tony hakumpa jibu linalo eleweka aliendelea kuongea.
"Unaweza ukanisaidia kunionyesha nyumba ya mtendaji au mwenyekiti wa kijiji"
Mama Mwanakombo aliendelea kuwa na maswali mengi kuhusu ujio wa polisi wale.
"Mtendaji wa kijiji nyumba yake ukivuka nyumba ile unayoiyona mbele yako, inayofuata ndiyo yake"
Alimuelekeza baba yule ambaye hakutaka hata kufahamu jina lake huku akiwa na wasiwasi kitendo kilichomfanya afunge mlango na kwenda kwa Stephano.
Alitembea haraka haraka, akaona anachelewa akaamua kukimbia huku khanga yake akiwa ameishika mkononi alipofika kwa Stephano alikaribishwa na kufuri ambalo lilikuwa linaning'inia mlangoni.
Nguvu zikamuisha akageuza na kurudi nyumbani kwake.
Sekunde chache tu, taarifa za ujio wa polisi zikasambaa kijijini pale Frank akashindwa kuvumilia akachukua simu yake na kumpigia Anna ambaye alikuwa nyumbani kwao.
"Hivi wewe ulimpenda Stephano ili uje kumuingiza matatizoni?"
"Mbona sijakuelewa unachokiongea frank"
"Hivi ninavyozungumza na wewe kwenye simu Stephano anasakwa na polisi, baba yako ndiye ambaye anaongoza msako huwo"
Anna alishangaa na kuendelea kuongea 
"najua mimi ndiyo mwenye makosa ila ni lazima nimsaidie Stephano manake yupo kwenye matatizo makubwa"
Alipomaliza kuongea maneno yale alikata simu na kuchungulia getini mlinzi alikuwa amekaa anasikiliza radio.
Akaumiza kichwa jinsi ya kumtoa mlinzi pale getini ili aweze kutoka nje akiri ikatumika ipasavyo, akarudi chumbani kwake na kuchukua nguo ambazo zilikuwa zimechakaa sana akaenda nazo nyuma ya nyumba na kuzichoma moto na kukimbilia tena dirishani kumuangalia mlinzi kama atanasa. Sekunde chache moshi ukatanda eneo lile na harufu ya nguo ikamshtua bwana Masunga ambaye alikuwa getini.
Aliamka haraka haraka na kwenda nyuma ya nyumba naye Anna akupoteza muda alitimua mbio kuelekea getini na kufungua mlango na kutoka nje ya nyumba.
Alikimbia kuku akiwa na hofu ya kufatwa na mlinzi.
Mlinzi alihangaika kuzima moto bila kufahamu kama kuna kitu kinaendelea.
Anna alikimbia huku akiwa anahema juu juu.
Akiwa amekaa juu ya Mnazi kwa macho yake alimuona mtendaji wa kijiji akiwa amefatana na polisi wakiwa wanakuja nyumbani kwake.
Hapo sasa ndipo alipoweza kupata majibu ya maswali ambayo alikuwa anajiuliza.
Mwenyekiti wa kijiji alifika mpaka kwenye nyumba ambayo anakaa Stephano na kusimama na kunyoosha kidole.
Stephano alijitahidi kusikiliza kwa makini lakini hakuna kitu alichoweza kusikia. Wakiwa bado wapo kwenye mazungumzo gafla Anna alifika eneo lile huku akiwa anahema kwa na kumnyooshea kidole baba yake na kuongea maneno makali.
Maneno yake yalimshangaza kila mtu,
Aliongea maneno yale huku akiwa anapiga kelele kitendo kilichomshangaza mwenyekiti wa kijiji, kelele zile zikaita majirani.
***********ITAENDELEA************
ANNA ANAZIDI KUMUINGIZA MATATIZONI STEPHANO
JE KIPI KITAENDELEA TUKUTANE SEHEMU YA KUMI YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA

No comments