WHY ME_________(08)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
Mzee alijibu kwa jazba kubwa na kumwambia
"Mimi ni baba wa binti ambaye ulimpa hii picha"
Aliitoa ile picha na kumuonyesha, Stephano alishtuka na uso wake ulionekana dhairi kuwa ulikuwa na wasiwasi, Mzee Tony akamuuliza swali lingine ambalo lilimpa maswali mengi sana Stephano.
SHUKA NAYO SASA
"Hii picha ni ya nani?"
Stephano alinyamaza kwa sekunde chache kisha akamjibu kwa sauti ya unyonge
"Ni yakwangu laki,,"
Kabla ajaendelea kuongea alikatishwa na maneno ya Mzee tony.
"Hayo mengine utaenda kuongelea huko na sio hapa"
Baada ya kumaliza kuongea maneno yale aliondoka na kumuacha Stephano kwenye sintofahamu kwani hata maneno ambayo alikuwa anayaongea mzee tony hayakuwa ya kawaida.
Stephano alinyanyua madumu yake na kuendelea na safari yake huku kichwani akiwa na mawazo mengi sana. Ikiwa yule ambaye amekuja na picha yake alikuwa mgeni machoni mwake, na picha ile ilikuwa ndani kwake hakuwahi kumpa mtu yoyote sasa leo hii picha yake ipo mikononi kwa mtu ambaye hamfahamu huku akionyesha vitisho vikari juu yake.
Mzee tony alirudi nyumbani na kukuta chai mezani, kwa hasira ambazo alikuwa nazo hakunywa hata ile chai moja kwa moja aliingia chumbani kwake na kubadirisha nguo na kuondoka bila hata ya kuongea na mtu yoyote.
Tumezoea kuona ofisi ya kata ndiyo inayoshughulika na kuwashikilia watu wenye makosa madogo madogo kabla hawajaenda ngazi za juu, pia wagambo ndiyo ambao wanahusika sana kwenye swala la ukamataji wa wahalifu.
Ila haikuwa hivyo kwa mzee tony, hakutaka ushilikiano wowote wa mtendaji wa kijiji wala mgambo,
aliondoka moja kwa moja mpaka kituo cha polisi ambacho kilikuwepo muheza mjini.
Alitopokelewa na polisi wa zamu na kusikilizwa malalamiko yake huku kila polisi akionekana kuwa makini sana, kabla ajamaliza kuongea polisi mmoja akadakia na kuongea kwa sauti ya juu.
"Mpaka hapo ulipo ongea inatosha mzee kwani kutembea na mwanafunzi adhabu yake inajulikana"
Mzee tony alitoa ile picha na kumkabidhi askari ambaye alikuwa karibu yake na kumwambia.
"kijana mwenyewe ndiyo huyu"
Baada ya kuonyesha ile picha polisi mmoja alishtuka ila hakujionyesha waziwazi, polisi mmoja akaongea kwa sauti
"Mzee swala la kumkamata huyo kijana ni kazi ndogo sana ila kwa sasa gari la polisi limeenda kijiji cha pili kuna tukio la uhalifu limefanyika hivyo tunaomba uvute subira kidogo likija tutaondoka, na ingekuwa vema zaidi ungetusubiri hapo nje"
Mzee Tony alitoka nje huku akiwa anaongea peke yake kama chizi au mtu alierukwa na akili.
Frank alikuwa anafanya usafi chumbani kwake gafla simu yake ikaita, alipoitazama hakuwa mwengine bali ni kaka yake, alipokea huku akiwa na furaha, walipenda sana kutambiana pindi timu zao kongwe za ulaya zinapokutana uwanjani frank alipokea simu na kuanza kuongea bila hata ya salamu
"Kesho nisiposhinda jezi yangu naichoma moto kwa hasira"
Kaka yake alicheka na kumwambia
"Sijakupigia simu kwa ajili ya mambo hayo ila kuna jambo muhimu sana nataka nikwambie"
Frank ambaye ni mtoto wa tatu wa Mzee philimoni alikuwa makini kumsikiliza kaka yake.
Afande peter alimuelezea mambo yote frank ambaye alibaki mdomo wazi muda wote.
Kitendo cha kaka yake kukata simu Frank alitimua mbio kitendo kilichomshangaza mama yake mzazi ambaye alikuwa nje anaosha vyombo.
Alifika kwa Stephano na kugonga mlango huku akiwa anahema sana, kitendo kilichomfanya ashindwe kuongea na kubaki anarudia rudia tu maneno, Stephano alimshangaa na kuanza kucheka kwa sauti ya chini.
"Hivi frank bado haujaacha huwo utoto wako"
Alipomaliza kuongea maneno yale akataka kuingia ndani ila Frank alimshika mkono na kumwambia
"Stephano umefanya makosa ndugu yangu"
Stephano alishangaa ila Frank akaendelea kuongea kwa jazba
"Ushaharibu ndugu yangu utampaje picha mtoto wa kike"
"Nani?"
Stephano aliuliza na Frank akaendelea kuongea
"Wewe umempa picha Anna na hivi ninavyokwambia baba yake Anna yupo muheza kituo cha polisi"
Stephano alishtuka na kujikuta ameshikwa na kigugumizi cha gafla
"we..we..we..we..wewe taarifa hizo amekupa nani?"
"Afande peter"
Stephano alimuangalia Frank na kumwambia.
"Frank mimi sijampa Anna picha ila masaa machache kuna tukio la kushangaza lilijitokeza kuna Mzee alinisimamisha na kunitolea maneno ya vitisho na kunionyesha picha yangu ambayo siku zote ipo ndani kwangu na kunihoji maswali ambayo sikuweza kupata ufumbuzi mpaka wewe ulivyokuja kuniletea taarifa hizo"
"Kama haujampa basi kaiba"
Stephano alinyanyua mikono yake na kuiweka juu ya kichwa chake na kuongea huku akiwa analia
"Frank unakumbuka tukiwa shuleni nilishawahi kukwambia kwamba yanayokuja mbele yangu ni zaidi ya haya sasa nadhani ushakuwa shahidi wa hili jambo"
Frank alinyamaza kwa dakika kadhaa kisha akamwambia
"Stephano hata ukisema tuanze kulaumiana itakuwa ni kazi bure cha kufanya tujue tunafanyaje"
"Frank tambua kuwa sina ndugu ambaye nikipelekwa polisi atakuja kunitoa, na huu ndio mwanzo wa kuishi kama mkimbizi"
Maneno yele yalizidi kumchanganya Frank ambaye alikuwa amenyamaza kimya huku akiwa anamuangalia Stephano ambaye alikuwa anaongea huku machozi yakiwa yanamtoka
Frank alinyamaza kwa sekunde chache kisha akamshika bega na kumwambia
"Stephano kinachotakiwa wewe pita njia nyingine na mimi nipite njia nyingine ila wote tukutane nyumbani halafu tutajua cha kufanya"
Stephano alianza kuingiwa na wasiwasi wa hali ya juu alianza kumtilia mashaka Frank.
Stephano alikataa kabisa kwenda kwa kina Frank,
Frank akamuangalia Stephano na kumwambia
"Tambua hapa kijijini hakuna mtu ambaye hakufahamu na usipojificha itakuwa ni rahisi sana kukamatwa"
Stephano alikaa kimya kwa dakika chache kisha akaendelea kukataa.
Mabishano yaliendelea baina ya wawili hao huku kila mmoja akiwa anataka achukue maamuzi yake.
Wakiwa wanaendelea kubishana gafla Frank simu yake ikaingia ujumbe mfupi alipoutazama alikuwa ni kaka yake alimwambia na kumuhimiza sana.
"Mwambie huyo rafiki yako akikamatwa itakuwa vigumu sana kutoka, kwani baba yake na huyo binti anaonekana hana asira sana, na hivi tunavyoongea muda sio mrefu tutawasili hapo kijijini"
Alipomaliza kusoma ule ujumbe alimkabidhi simu Stephano ambaye alisoma ujumbe huku akiwa anajiuliza maswali mengi sana kichwani mwake
Wakiwa wanajadiri cha kufanya Frank likamkuta wazo na kumwambia
"Kama una kiasi kidogo cha pesa jaribu kuondoka walahu kwa wiki mbili ili uweze kusikilizia"
Stephano alicheka kisha akaongea kwa Sauti ya kujiamini
"Hapa ndio kwetu nitabaki hapahapa na siendi popote.
Maneno yale yalimshangaza frank ambaye ndiye aliyemletea taarifa zile.
Stephano aliingia ndani na kutoka na mfuko ambao frank hakuweza kutambua ulikuwa na nini kisha akafunga mlango na kumtazama frank ambaye muda wote alikuwa amesimama tu bila kuongea chochote
"Frank nenda kaendelee na shughuli zako tutaonana baadaye"
Frank alishtuka na kumuuliza
"Sasa unakwenda wapi?"
Stephano hakujibu kitu chochote aliondoka na kuelekea balabalani kabla hajaivuka balabala mama ambaye alimchotea maji masaa machache yaliopita akamuita ili ampatie pesa yake kitendo cha kwenda kwa yule mama gari la polisi likasimama maeneo yaleyale Stephano akaliona kwa macho yake
**********ITAENDELEA***********
MAMBO YANAZIDI KUWA MATAMU
STEPHANO KWENYE MSAKO WA NGUVU KIJIJINI HAPO
TUKUTANE SEHEMU YA TISA YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA

No comments