soma hadithi hii ili uweze kuburudika


WHY ME_________(06)

Na:Stephano mwaimu
Contact_________ 0715293971
Ilipoishia
kumwambia
"Unataka nikamwambie baba yako, nakuomba rudi ndani"
Anna akaongea kwa sauti ya chini
"Kama hautaki sawa mimi nilikuletea zawadi"
Anna akaingiza mkono kwenye brauzi na kutoka na kitita cha pesa kitendo kilichomfanya mlinzi macho yamtoke.
SHUKA NAYO SASA
Mlinzi alimtazama Anna huku akiongea kwa sauti ya chini
"Unataka uwende wapi na kufanya nini?"
Anna alicheka kisha akamwambi
"Kuna rafiki yangu yupo hapo nje nataka nimpe chakula"
Baada ya kumaliza kuongea vile Anna alinyoosha mkono ishara ya kumkabidhi zile pesa, Naye alizipokea huku akiwa anatetemeka, Anna alizidi kuongea kwa sauti ya chini
"Hizi pesa nimekupa tu, ila zawadi yako ipo kesho mchana nitakupa"
Mlinzi badala ya kusikia maneno yale kutoka kwa Anna akazidi kupagawa na kumwambia
"Sawa nakufungulia ila usichelewe"
"Mimi sichelewi hata dakika tano azifiki nitakuwa nisharudi"
Baada ya kuambiwa maneno yale bila ya kuchelewa akafungua geti Anna akatoka nje na safari ya kwenda kwa stephano ikaanza.
Akiwa amechoka kutokana na kazi ngumu anazozifanya Stephano alikuwa amejilaza kitandani gafla mlango ukagongwa akashtuka na kumuitikia, Alinyanyuka na kwenda kufungua hakuwa mwengine alikuwa ni Anna
"Wewe umefata nini saizi"
Anna alishtuka na kumjibu
"Swali gani hilo ambalo unaniuliza, sijafata kitu ila nimekufata wewe"
Stephano alishusha pumzi na kumwambia
"Karibu"
Anna bila ya hiyana kwa mara ya pili akaingia tena ndani na kuketi kitandani, Kabla ya kuongea kitu Stephano akamuuliza
"Humo kwenye hotpot kuna nini?"
"Nimekuletea chakula"
Stephano alikaa kimya kisha akajiongelea mwenyewe kimoyomoyo
"We mwanamke ujio wako unanitia mashaka sana haya ni matatizo ambayo tunatafutiana"
Alikaa kimya kama sekunde hamsini huku akiwa ameshikilia mlango Anna akamuuliza
"Unawaza nini"
"Anna nahisi wewe unataka kunitafutia matatizo mimi"
Anna alishangaa na kumuuliza
"Kivipi"
"Wewe ni mwanafunzi saizi haupo nyumbani unadhani wazazi wako wakigundua kuwa wewe haupo nyumbani hauwoni kuwa lazima litokee tatizo hapo"
Anna alicheka na kumuangalia Stephano kisha akaliweka hotpot kitandana na kunyanyuka na kumwambia.
"Leo nipo peke yangu nyumbani na kwanini uwe na mawazo hayo mimi sio mtoto mdogo nakuomba ondoa hofu"
"Anna naweza kukwambia nilikuwa na njaa lakini imeisha gafla nimejiona nimeshiba kutokana na ujio wako"
Alipomaliza kuongea maneno yale alienda kukaa kitandani kisha akamuuliza
"Kwahiyo ni kipi hasa kilichokuleta usiku huu"
"Kwani itakuwa nimefanya vibaya tukilala wote"
Stephano akashtuka na kumeza mate kisha akacheka na kumwambia
"Hivi sijasikia au,,, inamana ujio wako ni wakuja kulala kwangu"
"Ndio"
"Sasa mbona haujabeba shuka"
Anna alishangaa kuambiwa vile kuna kitu akataka kumuuliza ila roho ikasita na kuamua kumjibu
"Tutajifunika wote hiyohiyo"
Stephano alitamani amwambie aondoke ila akikumbuka ahadi ambazo alimuahidi kwa mdomo wake mwenyewe anashindwa.
Mlinzi alikaa mpaka saa tano bila mafanikio yoyote woga ukaanza kumuingia na kujikuta anajuta kumfungulia na kujililia mwenyewe huku akisema
"Tamaa ya pesa ndio ambayo imeniponza ni lazima nimwambie baba yake manake likitokea tatizo ni lazma nilaumiwe mimi,
ila nitamuanzaje sasa naona kama kibarua kishaota nyasi"
Usiku ule ndio ilikuwa siku ya kwanza ya Anna na Stephano kukutana kimwili.
Mlinzi alivumilia mpaka saa nane kasoro uzalendo ukamshinda na kwenda kumuamsha Boss wake mzee tony na kuanza kujiuma uma meno kitendo kilichomfanya Mzee tony asimuelewe anaongea nini kwani alikuwa analia tu badala ya kuongea.
"Masunga vipi mbona umeniamsha usingizini alafu unachokiongea akieleweki vipi kulikoni"
Ikabidi ajikaze na kumwambia ukweli
"Boss najua nimekosa ila nisamehe Anna aliniambia anakwenda kwa rafiki yake na hatochelewa kurudi ila mpaka sasa hajarudi"
Mzee tony alishangaa na kumwambia Anna si aliingia chumbani kwake kwenda kulala"
"Apana boss alitoka"
Mzee tony ili apate uwakika zaidi aliingia ndani moja kwa moja mpaka chumbani kwa Anna na alipofungua mlango ulikuwa umefungwa na funguo na alipochungulia kwenye tundu la funguo tundu lilikuwa halina funguo, Alitikisa kichwa na kwenda chumbani kwake kuchukua funguo za akiba na kuja kufungua, kweli chumba kilikuwa cheupe.
Mzee tony alitoka nje na kumuuliza mlinzi "Kaondoka saa ngapi"
"Kwa kukadilia ilikuwa kama saa nne"
"Hivi nilishakuonyaga mara ngapi kuhusu kuwa makini hapa getini?"
Mlinzi alinyamaza kimya huku akiwa anatetemeka na mzee tony aliendelea kuongea kwa hasira.
"Huwo ni uzembe wa hari ya juu, inaonyesha dhahiri kuwa haupo makini na kazi yako"
"Nisamehe boss mimi nimejilalia zangu unanisumbua, au kazi imekushinda, kama imekushinda sema nitafute mtu mwengine"
"Apana boss nakuahidi sitarudia tena boss wangu"
Aliingia ndani kwa hasira na kuwasha simu na kumpigia Anna lakini simu yake ilikuwa haipatikani.
Alichokifanya ni kupanda kitandani na kuendelea kulala.
Akili haikuwa sawa kabisa baada ya dakika tano alinyanyuka na kwenda sebureni.
Stephano alikuwa na mashaka sana juu ya Anna ukiangalia mazingira ambayo alikuwa anaishi ni mazingira ambayo hakuna kitu ambacho alikuwa anakosa kwa wazazi wake.
Majira ya saa kumi Stephano alimuamsha Anna na kumwambia
"Ningekuomba uwende kwenu manake nataka niende kumalizia kazi ya watu"
"Saizi?"
"Ndio"
Anna aliguna na kumwambia
"Unajua kuna muda mwengine inatakiwa uwe unajionea huruma kazi ambazo unafanya ni ngumu sana na malipo yake ni madogo sana hivyo inaitaji upate muda mwingi wa kupumzika"
Stephano alicheka na kumwambia
"Anna tanzania ya sasa unadhani nisipojishughulisha nitakula wapi, ukizingatia nipo mimi kama mimi sina ndugu wala jamaa"
Anna alimuangalia Stephano na kumwambia
"Najua unafanya hivyo ili uweze kupata pesa ambayo itaweza kukidhi mahitaji yako ila bado pesa unayoipata ni ndogo sana, leo jioni nitakutafuta kuna kiasi cha pesa nitakuletea, sijapenda hata kidogo ufanye ile kazi"
"Lakini tambua kuwa akiri za kupewa ni vizuri ukichanganya na zakwako"
"Unamaana gani?"
"Nilikuwa namaanisha hivi yanipasa nisiangalie upande mmoja kwani wewe ni binadamu kama mimi, na yule anayebebwa mgongoni hawezi kulalamika amechoka kwa sababu amebebwa"
"Ata kama ila ile sio kazi nzuri kiujumla ningekuomba uwachane nayo na si kinginecho"
Stephano alinyanaza kimya na Anna akamwambia
"Narudi nyumbani ila wewe pumzika"
Anna alinyanyuka na kuchukua picha ya Stephano iliyokuwa imekaa mezani bila ya mwenyewe kujua na kuondoka.
Alifika nusu ya safari ndipo akakumbuka kuwa kuna kitu amesahau alifikilia na kusema.
"Nitarudi kukipambazuka"
Muda mchache alikuwa amefika nyumbani kwao aligonga geti polepole mlinzi alikuwa makini sana kwani masikio yake yote yalikuwa ameyaelekeza getini, aliposikia geti limegongwa akafungua na kuchungulia nje macho yake yakagongana na macho ya Anna yaliojaa aibu tele na kumuuliza
"Unatoka wapi saizi"
Anna hakujibu kitu, Masunga alimpisha na kumwambia
"Ingia ndani utajua mwenyewe na balaa lako na usije ukanifukuzisha kazi shika pesa zako urafiki na wewe sitaki"
Anna alishtuka na kumwambia
"Inamana masunga hizi pesa hauzitaki"
"Nishakwambia ondoka nazo mimi sizitaki"
Anna akazichukua ili kuepusha kelele na kuanza kuingia ndani huku akiwa anawasi wasi wa kuonekana na baba yake.
Alifungua mlango na kuingia ndani taratibu kisha akajitahidi kuufunga taratibu alipomaliza kufunga akaendelea kunyata kuelekea chumbani kwake, alipokaribia kwenye mlango wa chumbani kwake gafla taa zote za mule ndani zikawashwa akashtuka na alipogeuka pembeni uso wake ulitazamana na baba yake mzazi.
***********ITAENDELEA***********
ANNA ATAMUELEZA NINI BABA YAKE MZAZI AU SIRI NDIO ISHAFICHUKA
TUKUTANE SEHEMU YA SABA YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA
PIA ENDELEA KUNIFATILIA
facebook/ Stephano wa hadithi
instagram/uwanja_wa_simulizii

No comments